Log inLog Out
For YouNewsEntertainmentRelationshipLifestyleBusiness
Mafisi wameza mate! Shahidi katika kesi dhidi ya Waiguru awakosesha mafisi usingizi

Moruf

Jun. 25, 2020

Kesi ya Gavana wa Kirinyaga Ann Waiguru katika seneti iliacha Wakenya wakiwa na hisia mseto kuhusiana na uzito wa mashtaka dhidi yake.
Kuna waliohisi kuwa mashtaka hayo ni mazito na anafaa kutimuliwa na seneti  kama walivyofanya wawakilishi wadi wa bunge la kaunti ya Murang’a huku wengine wakitaka yatupiliwe mbali.
Hata hivyo, kwa mafisi waliokuwa wakifuatilia mahojiano hayo, hawana ufahamu wowote kuhusu mashtaka yaliyowekwa wazi pale. Kwa wao, ni shahidi Goody Gor tu waliweza kufuatilia simulizi zake pale huku wakimezea mate kwa sababu ya sura yake ya kuvutia.
Gor ndiye katibu wa muungano wa wahudumu wa afya (KMPDU) katika eneo la Kati.
Mafisi walifurahia ukakamavu wake na mazungumzo yake wakati wa kuelezea matatizo ya sekta ya Afya katika eneo la Kati. Licha ya kuonekana mdogo kwa umri, ameweza kuchaguliwa kama katibu kwenye muungano huo.
Binti huyo alihitimu na shahada ya udaktari na sasa ni miongoni mwa sauti muhimu katika masuala ya matibabu.
Mafisi wamekuwa wakitaka kumjua zaidi binti huyo na upekuzi wetu umeonyesha kwa kweli ni mtu anayependa kujipa raha Kwenye mtandao wake, ameweka picha za kuvutia ambazo zitawapa mafisi tamaa zaidi.
Kwa hakika yeye ni mkamilifu wa kile huarifiwa kama ‘beauty and brains’ na wengi watatamani wajipate kwenye mikono yake.
Sura yake iliwafutia wengi wakati wa kusikizwa kesi ya Waiguru, huku wengi kwenye mitandao ya kijamii wakisema kuwa ni mrembo kupindukia.
MHARIRI: DAVIS OJIAMBO
0
Comments
Sign in to post a message
You're the first to comment.
Say something
Recommend
Log in