Log inLog Out
For YouNewsEntertainmentRelationshipLifestyleBusinessTechnology
Mbunge Babu Owino Achemsha Mtandao Baada Kutaka Mshahara Wake Upunguzwe, Asilimia 50

Kuloba KE

March. 26, 2020

Wanamtandao walisema Babu anatafuta umashuhuri wa kisiasa wakati huu wa janga la corona. Walimtaka kwanza alipe bili ya hospitali ya DJ Evolve kabla ya kusema yuko tayari kukatwa mshahara wake. Wazazi wa Evolve wamekuwa wakiteta kuhusu hali ya mtoto wao pamoja na kuongeza kwa bili ya hospitali.
 Babu Owino alidaiwa kumpiga risasi Evolve walipokuwa kwenye klabu moja jijini Nairobi Mbunge wa Embakasi Mashari Babu Owino aliwasha mtandao wa twitter Jumatano, Machi 25 baada ya kusema yuko tayari kukatwa mshahara wake kwa asilimia 50. Mbunge huyo alitangaza hilo baada ya Rais Uhuru Kenyatta kusema kuwa yeye na naibu wake William Ruto watakatwa asilimia 80% ya mshahara wao kutokana na coronavirus. 
Wakenya walimlima mbunge huyo wakisema kuwa tangazo lake ni kutafuta umashuhuri wa kisiasa na wala si kusaidia lolote wakati huu wa janga la coronavirus. Wanamtandao walimtaka Babu kulipa bili ya hospitali kwanza ya DJ Evolve aliyempiga risasi na kufanya alazwe hospitali kabla ya kusema anataka mshahara wake ukatwe. Wakenya walimtaka Babu asimamie bili hiyo kwani wazazi wa Elvolve wamekuwa na machozi kuhusu hali ya mtoto wao pamoja na bili ya hospitali. 
0
Comments
Sign in to post a message
You're the first to comment.
Say something
Recommend
Log in