Log inLog Out
For YouNewsEntertainmentRelationshipLifestyleBusiness
Chuo Kikuu Cha Maseno Chafungwa Kufuatia Mgomo Wa Wanafunzi

Bertillar

Dec. 02, 2019

Chuo Kikuu cha Maseno University kimefungwa kwa muda baada ya wanafunzi kugoma mnamo Jumapili, Desemba 1.
Kwa mujibu wa taarifa, wanafunzi hao waliandamana kulalamikia katika kile walikitaja kama utovu wa usalama chuoni humo na visa vya ubakaji.
Katika taarifa kutoka kwa Chansela wa chuo hicho, Julius Nyabundi, alisema hatua hiyo ilifikiwa siku ya Jumapili jioni na Seneti baada ya wanafunzi kukosa kuhusisha uongozi wa chuo hicho kuhusu njia mbadala ya kusuluhisha suala hilo.
"Kufuatia mgomo wa wanafunzi kwa madai ya visa vya ubakaji vilivyoripotiwa na wanafunzi wanaoishi nje ya chuo, wakazi na wanafunzi kushindwa kuhusisha uongozi wa chuo kwa mjadala wa kusuluhisha suala hilo, Seneti ilikutana Jumapili, Desemba 1, saa moja jioni na kuamua kufunga chuo hiki kwa muda.
Wanafunzi wanaagizwa kuondoka chuoni kufikia saa moja unusu leo, Jumapili, Desemba 1," ilisoma taarifa hiyo.
Hata hivyo, hatua ya chuo hicho imekashifiwa vikali na Wakenya wengi ambao walidai kuwa waliharakisha kufikia uamuzi huo na kuhatarisha maisha ya wanafunzi.
0
Comments
Sign in to post a message
You're the first to comment.
Say something
Recommend
Log in