Log inLog Out
For YouNewsEntertainmentRelationshipLifestyleBusiness
BBI: Mashirika Ya Kamari Ya Kibinafsi Kuharamishwa

Bertillar

Nov. 29, 2019

Kampuni za kamari za kibinafsi huenda zikapigwa marufuku nchini endapo ripoti ya BBI itatekelezwa na serikali.
Badala yake, ripoti hiyo inapendekeza kubuniwa kwa kampuni moja itakayomilikiwa na serikali kuendesha biashara ya kamari.
“Kampuni za kamari za kibinafsi zinazidi kuwafanya vijana kuwa maskini hohehae. Jopo hili linapendekeza kubuniwa kwa kampuni ya serikali ambalo mapato yake yatatumiwa katika kuboresha maisha ya vijana, michezo, utamaduni na shughuli nyinginezo za kijamii,” inasema ripoti.
Kampuni za kamari Sportpesa na Betin tayari zimesimamisha operesheni zao nchini kwa madai kuwa zilihangaishwa na serikali.
Sportpesa na Betin zilikuwa miongoni mwa kampuni 19 za kamari zilizopokonywa leseni kwa kukwepa kulipa ushuru.
Jopo hilo linataka serikali kubuni sheria kali ya kudhibiti mikopo inayotolewa kwa njia ya simu kutokana na kile linachosema ‘inawaletea’ umaskini Wakenya.
Jopokazi la BBI pia limeonya serikali dhidi ya kuchukua mikopo kutoka katika mataifa ya kigeni.
“Usiwatwike watoto wetu mzigo mzito wa madeni kwani watateseka katika siku za usoni. Kizazi cha sasa hakifai kuumiza kizazi kijacho,” inaonya ripoti hiyo.
Jopo hilo pia linapendekeza vijana wanaoanzisha biashara wasitozwe ushuru kwa kipindi cha miaka saba.
0
Comments
Sign in to post a message
You're the first to comment.
Say something
Recommend
Log in