Log inLog Out
For YouNewsEntertainmentRelationshipLifestyleSportTechnology
Walinzi wa kaunti wazuia Musalia Mudavadi na Moses Wetangula kuhudhuria mkutano wa wazee wa luhya

Turk Naid

July. 11, 2020

Jumamosi,11,Julai walinzi wa kaunti ndogo ya Emuhaya walisimama malangoni mwa mbunge Omboko Millemba ili kuzuia kiongozi wa chama cha ANC na Ford kenya kuingia katika eneo hilo.
Kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi na mwenzake kiongozi wa ford kenya Moses Wetangula walikuwa wahudhurie mkutano huo nyumbani mwa mbunge huyo mtaa wa Emuhaya.
Omboko ni mbunge wa Emuhaya na pia mwana chama wa chama cha ANC.
Mudavadi na Wetangula walitarajika kuktana na viongozi na wazee wa magharibi ilil kujadili umoja wa waluhya katika eneo hilo.
Wikendi hii wawili hao walitarajiwa kuendea katika kaunti ya Kakamega na Vihiga.
Musalia na Wetangula wikendi iliyopita walikuwa katika maeneo ya Trans Nzoia na Busia walipoidhinishwa na wazee wa mkoa huo kuleta umoja kwa wananchi wa luhya.
Walipoanza mkutano wao timu nyingine iliyo ongozwa na gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya na waziri Eugene Wamalwa walipitia maeneo hayo waliposema mkutano wao ni wa ‘unity and development agenda’.
Mbunge wa Lugari Ayub Savula ambaye alikuwa ameandalia Mudavadi na Wetangula mkutano wa jumapili alikuwa na haya ya kusema.
“Viongozi wa mkoa wa Luhya ambao wanatambulika na kufahamika ni Moses Wetangula na Musalia Mudavadi wale wengine hawajulikani.”
Viongozi hao walisema kuwa mkutano huo utahudhuriwa na watu wachache na wala hautazidi saa moja, walisema kuwa watahahakikisha kuwa kuna nafasi ya mita moja kama vile ilivyoagizo la wizara ya afya ili kukomesha kusambaa kwa virusi vya corona.
0
Comments
Sign in to post a message
You're the first to comment.
Say something
Recommend
Log in