Log inLog Out
For YouNewsEntertainmentRelationshipLifestyleSportTechnology
COVID 19: Amerika yatoa notisi ya kujiondoa WHO

Hoa

July. 08, 2020

Rais wa Marekani  Donald Trump hatimaye ametoa notisi ya kujiondoa kwa Marekani kutoka  shirika la Afya Duniani WHO.
Rais huyo aliweka wazi lengo lake mwezi Mei , akililaumu shirika hilo la WHO kuwa chini ya udhibiti wa China kufuatia mlipuko wa virusi vya corona.
Licha ya wito kutoka kwa Muungano wa Ulaya na wengine, alisema kwamba ataiondoa Marekani kutoka katika kitengo hicho cha UMoja wa Mataifa UN na kupeleka ufadhili wake kwengineko.
Rais wa Brazil Bolsonaro apatikana na virusi vya corona
Kufikia sasa ametoa ilani kwa UN na bunge la Congress kuhusu malengo yake, ijapokuwa mkakati huo unaweza kuchukua kipindi cha mwaka mmoja.
Stephane Dujarric, msemaji wa katibu mkuu wa UN, alithibitisha kwamba Marekani imetoa ilani kuhusu kujindoa kwake kuanzia tarehe 6 Julai 2021.
Seneta Robert Mendez , kiongozi wa Democrat katika kamati ya masuala ya kigeni, pia aliandika katika twitter: Congress imepokea notisi kwamba POTUS  amejiondoa rasmi katika shirika la Afya Duniani WHO katikati ya mlipuko wa corona.
”Inaiwacha Marekani ikiugua na pekee”
Afisa mkuu wa utawala wa rais Trump aliambia CBS News kwamba Washington ilielezea mabadiliko inayohitaji WHO kufanya na kujadiliana nayo moja kwa moja , lakini Shirika hilo limekataa kuchukua hatua.
“Kwasababu wamefeli kufanya mabadiliko yaliotakiwa , hii leo tutavunja uhusiano wetu , afisa huyo alinukuliwa akisema.
Joe Biden, ambaye atampinga rais Donald Trump katika uchaguzi wa mwezi Novemba , alituma ujumbe wa Twitter akisema: Katika siku ya kwanza kama rais, Nitairudisha Marekani katika WHO na kuimarisha uongozi wetu duniani.
COVID 19: Visa vya walio na virusi vya corona sasa ni 183 na kufikisha 8,250
Marekani ndio mfadhili mkuu wa shirika hilo, likitoa $400m (£324m; €360m) mwaka 2019, takriban asilimia 15% ya bajeti yake kwa jumla.
Chini ya uamuzi wa Congress 1948, Marekani inaweza kujiondoa lakini lazima itoe notisi ya mwaka mmoja na italazimika kulipa fedha inazodaiwa , ijapokuwa haijulikani ni upi msimamo wa Trump kuhusu hilo.
Bwana Dujarric alisisitiza kuwa masharti hayo ni lazima yaafikiwe. Kujiondoa huko kutagusia uwezo wa kifedha wa shirika hilo na hatma ya mipango yake kukuza afya na kukabiliana na magonjwa.
0
Comments
Sign in to post a message
You're the first to comment.
Say something
Recommend
Log in