Log inLog Out
For YouNewsEntertainmentRelationshipLifestyleBusinessTechnology
Jamaa Mmoja Aaga Dunia Katika Basi La Chania Akielekea Mombasa

Mary KE

March. 24, 2020

Polisi wameanzisha uchunguzi ambapo jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 30 aliaga dunia Jumatatu, Machi 23 asubuhi kaunti ya Makueni. Kulingana na polisi, marehemu, Fredrick Mbachu Mwakima alikuwa katika basi alipoanza kukohoa kabla ya kuzirai ghafla na kuaga dunia.
Basi hilo la kampuni ya Channia Cool lilikuwa linaondoka Nairobi kuelekea Mombasa wakati kisa hicho kilipotokea ambapo gari hilo lilikuwa limesimama katika hoteli ya Taleh, Kibwezi .
Inasemekana maafisa wa afya katika eneo bunge la Kibwezi waliwasili eneo hilo wakauchukua mwili wa mwenda zake na kunyunyiza dawa katika basi hilo.
-Tuko
0
Comments
Sign in to post a message
You're the first to comment.
Say something
Recommend
Log in